TPB POPOTE "Benki Yako, Mikononi Mwako"
TPB POPOTE ni huduma inayotolewa na Benki ya Posta Tanzania, inayomuwezesha mteja kupata na kujua mambo au taarifa mbalimbali zinazohusiana na akaunti yake wakati wowote na mahali popote kwa kupitia simu yake ya mkononi.
MADHUMUNI YA HUDUMA YA TPB POPOTE
Kuwajengea wateja tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya mipango ya maendeleo na mahitaji mengine ya dharura ya kifedha
Kuwarahisishia wateja kupata taarifa za akaunti zao pamoja na kusafirisha fedha
Kuwarahisishia wateja kulipia huduma mbalimbali (Mafaa)
JINSI YA KUJIUNGA HUDUMA YA TPB POPOTE
Kwa wateja wapya: Kwanza ni lazima mteja awe na akaunti katika Benki ya Posta Tanzania kama vile QUICK, PSA, WADU au CALL
Mteja anatakiwa kujaza fomu ya kusajili inayopatikana katika tawi lolote la Benki ya Posta au wakala wa Benki ya Posta Tanzania.
Kisha fomu hiyo ya usajili itaingizwa kwenye mfumo wetu wa mawasiliano ya kibenki na kisha mteja atapata ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi akitarifiwa juu ya kukubaliwa pamoja na kupewa namba ya siri ambayo atakuwa akitumia kila anapohitaji kupata au kutumia huduma ya TPB POPOTE.
MANUFAA YA HUDUMA YA TPB POPOTE
Uwezo wa kujiwekea akiba mahali popote wakati wowote.
Kupata taarifa zinazohusu akaunti yako mahali popote wakati wowote.
Kulipia huduma mbalimbali kama vile LUKU, MUDA WA MAONGEZI HEWANI, MAJI n,k. mahali popote wakati wowote.
Kusafirisha fedha kwa haraka na usalama zaidi mahali popote wakati wowote.
Kupata taarifa maalum (NOTIFICATIONS) kila fedha inapoingia au kutoka kwenye akaunti yako.
MENGINEYO KUHUSU YA HUDUMA YA TPB POPOTE
Hakuna gharama ya kujiunga.
Inatumika katika aina zote za simu za mikononi.
|